Dizasta Vina - Achia jala feat. Kaa la moto


Lyrics

Oya
Mwela alikuja nikampiga sound mbumba mbaya
Siwezi lala down town naitunza kaya
Niko around ninavunja taya
Michongo kibao town wana hawakuvuta waya
Achia jala
Ni heri kuyashinda majaribu
Ila kufeli ni kushindwa kujaribu
Baba alifeli siwezi feli pia
Namiliki jina la ukoo sio sheli dia
Siwezi lala njaa itanigaraza
Kwahiyo usiniletee risala achia jala kwanza
Sina kazi nimedandia ndala
Alafu unanikazia fala
Bro achia Jala
Hauna shida ndo' maana unapendeza
Alafu unaniambia hauna fedha
Sikupi kichaka sikupi hata stata  utakimbia, 
Achia jala ntakupiga mitama utajifia
Sikupenda kuwa vikundi vya wahuni, 
Nilikuwa madini ambayo hauyakuti vitabuni, 
Nilikuwa mtu kabla enzi zangu
Haya maisha yangu ni kitabu na hii ni peji chafu, 
So achia jala
Dingi mwenyewe alitoboka
Madeni kama dhambi milele nakokota 
Na alipodondoka nikarithi shida
Ndio maana Kuelewa mtu lazima uelewe alipotoka
So, Achia jala
Sichezi kamali na washua
Nitakupiga kabali nitakuua, sikuachii hata ukisali
Matumaini yako mbali 
Nami nipo katikati ya bahari Na mashua 
Hauwezi kuwa mtoto ukishazaa
Nina mtoto sasa, sitaki kuuza ndoto ka bidhaa
Mwanzo nilikuwa na ndoto na iling'aa
Lakini bahati mbaya mtoto hawezi kula ndoto ikija njaa
Nilipenda kuwa rubani
Ila mambo ni makubwa ukubwani
Nikaishia kuwa mkulima fani niliyofunzwa nyumbani
Kabla shamba halijakumbwa tufani
So achia jala
Nimekufata tangu Benki najua kuwa una cash
Uliingia ukiwa empty ukatoka na mabegi
Una-act kama Ndezi
Unaniletea undezi nitakuletea ushenzi wewe
Nilichora plan na sikupiga mchele
Wenzangu wa mtaani ni'shazika tele
Najua unahesabu time si ujaribu kurun sijui
Nimeshika gun nitakuchezea shere
Achia jala, 
Siwezi kudanganya kuhusu
Haya Madusko hatuwezi kugawana nusu
Usihubiri sisadiki maadili
Maisha yenyewe mafupi na hatuishi mara mbili
Achia jala
Mbunge halijui jina langu
Ramani ya jiji haisanifu  njia zangu
Hawajivunii ndugu zangu, Miungu haisikii sauti yangu 
Niko peke yangu mimi na gun yangu
Nitaku pah pah 
Kisha unione mamluki 
Nitakuchezesha mabuzuki
Nishafungwa mara tatu nimetoa roho nne
Utakuwa wa tano, so jaribu kutoka nduki nikuonyeshe 
Nipo kazini so achia jala 
Nitakutia ngwara ufe
Mafanikio ni kwa wale majasiri
Walio tayari kusubiri ni makupe
Nisikize brother
Ni'shafanya mamziki
Sikuvutia kukusanya mashabiki
Naogopa kuwa begi nishazika marafiki 
Nilishalala na maiti nishajiuza kwa shangingi
Nishafunga mahirizi, nishakula mamizizi
Nishafuga Jinamizi mamisuba nikasizi
Nishakuzwa na waizi waliokuzwa na machizi waso....
Mama ananiona failure for life
Na ninamisi kumbatio la wife
Mkwe ananiona bwege, napeleka nuksi malangoni pake
Shemeji ananiona sio type 
So achia jala, nitakubia roho nipe jala
Usinizoee usinipe gwara
Unahisi sina maadili ninafata mkumbo bwege
huwezi kuwa consious ukiwa tumbo empty
Achia jala
Sijarithi mali ili nizichunge kama zako
jala ziko mbali nizifuge Kama zako 
Wajomba masadali sio wabunge kama wako
Sijaenda shule yako... 
I'll fucking shoot you, Achia jala
Nimeshindwa leo sio kwamba nilisinzia jana
Sijakwambia kwamba alisinzia baba
Hakujua mkwanja ni maua mazuri yanafifia ghafla 
Achia jala

Hey, so sad hunijui boy, am not of your Calibre
Usituone tu tajiri, wengi tuna suck blood ki-Cannibal.
Msimamo kitaliban, na roho ya kijahidina.
Kama mbwai mbwai ndio utajua mi kikosi kama Pina.
But I won't choose that hata ka' niko street smart.
nna-pure fact nahisi we ni mgonjwa unahitaji meds. 
Mental disturbed maybe afya ya akili.
Na uko so bitter it's not healthy unapoteza asili.
Hata mi nilihaso man same thing na Bakhresa.
Niliogopa pressure sikutafuta demu ilikua p.......

0 Comentários